CCPM yaishukuru Meridianbet kwa kugusa maisha ya wazee wanaolelewa kituoni hapo kwa kutoa msaada wa vyakula na vifaa vya usafi.
Kwa namna ya kipekee kabisa, kituo cha kulea wazee cha The Community Centre for Preventive Medicine kilichopo jijini Dar es Salaam, kimetoa shukrani zake za dhati kwa kampuni ya ubashiri ya Meridianbet kwa moyo wao wa kujitolea kupitia msaada wa vyakula pamoja na vifaa vya usafi binafsi. Kitendo hiki kimeleta faraja kubwa kwa wote wanaopatikana katika kituo hiki.
Miongoni mwa mahitaji yaliyowasilishwa kituoni hapo ni mchele, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za unga na sabuni za vipande pamoja na vifaa mbalimbali vya usafi binafsi. Msaada huo una umuhimu mkubwa kwa taasisi hiyo kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo, huku wazee wakihitaji mazingira safi, salama na chakula bora katika hatua hii ya maisha yao.
Uongozi wa kituo cha The Community Centre for Preventive Medicine umepokea kwa furaha kubwa sana msaada huu kwani umegusa moja kwa moja changamoto ya uhaba wa vyakula na vifaa vya usafi inakikabili kituo hiki.
Wakiwa kituoni hapa, wawakilishi wa Meridianbet wamepata wasaa wa kuongea na wazee wanaolelewa kwenye kituo hiki na kuweza kutambua namna hali ya maisha ilivyo kituoni hapa, ikiwemo changamoto wanazozipitia.
Ulikua ni wasaa mzuri kwa kila mtu kituoni hapa kwani hali ya mazungumzo ya karibu, kucheka na kubadilishana mawazo ni jambo lililogeuza makabidhiano hayo kuwa tukio la upendo na mshikamano na kuonyesha kwamba jamii inapoungana, changamoto zinaweza kupunguzwa na watu wanaohitaji msaada wanaweza kupata matumaini mapya.
Kwa mara nyingine tena, Wanacommunity Centre for Preventive Medicine tunasema asanteni Meridianbet kwa kuwa sehemu ya furaha hii.
Jisajili mtandaoni, na kwa wale wa USSD na vitochi piga, *149*10#. #meridianbettz #kasinoyamtandaoni #slotimachine #ushindimkubwa #titanroulette #oddskubwa.


